Friday, May 25, 2012

Mambo 5 ambayo Watanzania wanayakataa na hawatovulimia tena chini ya CCM

Posted: 25 May 2012 10:28 AM PDT
Na. M. M. Mwanakijiji

Nimejaribu kutafakari kwanini kuna wimbi la watu kuikataa CCM na serikali yake kwa nguvu zaidi wakati huu kama ilivyokuwa mwaka 1995. Miaka mingi imepita lakini wakati mwaka 1995 ilikuwa kwa kiasi kikubwa ni kutumia uhuru wa kujiunga na chama kingine zaidi ya CCM safari hii kuna kitu tofauti kinajionesha wazi. Watanzania kwa maelefu – mijini na vijijini, wazee kwa vijana, wake kwa waume – wameamua kuiambia CCM “Bye Bye” na kujiunga kwa mbwembwe kwenye CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO. Nilipotafakari zaidi mang’amuzi haya mapya yanayoendelea nimejikuta nikirudi nyuma zaidi karibu miaka hamsini iliyopita.
Vitu vile vile vilivyowafanya Watanganyika na Waafrika kwa ujumla kuukataa ukoloni na serikali yake vimeanza kukataliwa tena na safari hii si dhidi ya ukoloni bali dhidi ya utawala ambao umegeuka na wenyewe na mwelekeo wa ukoloni usiopingika. Mambo haya matano manne kati yake yanajulikana sana kwani yamekuwepo katika tangazo la Azimio la Arusha la mwaka 1967 na ambalo ukweli wake bado unasimama.
Katika Azimio la Arusha tulitangaza hivi: Tumeonewa kiasi cha kutosha, tumenyonywa kiasi cha kutosha, tumenyanyaswa kiasi cha kutosha na tumepuuzwa kiasi cha kutosha… Ni unyonge wetu ndio uliotufanya tuonewe, tunyonywe, tunyanyaswe na tupuuzwe. Sasa tunataka mapinduzi ili tusionewe, tusinyanyaswe na tusipuuzwe tena!” Hivyo mambo manne ya kwanza ambayo Watanzania wanayakataa ni kuonewa, kunyonywa, kunyanyaswa na kupuuzwa. Tuyaangalie haya kidogo:

1. Tumeonewa
Watanzania wameamua kukataa kuonewa na watawala wao. Kuonewa huku kunakuja kwa aina nyingi sana lakini kubwa ni ile hisia ya tofauti kati ya watawala na watawaliwa ambapo watawala ambao kutokana na nafasi zao wanajiaminisha kuwa wanaweza kufanya lolote, kwa yeyote aliye chini yao. Mifano miwili iko wazi sana kuwakilisha hili. Wengi mnakumbuka yule DC aliyemzaba kibao baba wa watu mbele za watu na hakukemewa na Rais Kikwete wala viongozi wengine. Wapo watu wengi sana ambao wamejikuta wakionewa na watawala iwe katika ajira, biashara au hata nafasi tu. Matokeo yake Watanzania hawa wamejikuta wakilazimika (sijui kama ni sawa kuita kulazimika au kulazimishwa) wanatafuta kujipendekeza kwa watawala hao ili ‘mambo yao yawanyokee’.
Ni uonevu wa kiutawala ambao unalazimisha wananchi wa kawaida kuwa kama vijakazi mbele ya watawala. Ni uonevu unaowafanya watawala waweze kutoa maagizo yoyote kwa sababu ya utawala wao. Tumeona watu wetu walivyohamishwa kwa nguvu sehemu mbalimbali ili kupisha ‘wawekezaji’ tumeona mahali ambapo watu wamenyang’anywa maeneo waliyokuwa wanalima mazao ya chakula ili waje watu kulima mazao ya ‘mafuta’! Sasa Watanzania hawa wameamua kukataa kuonewa tena!

2. Tumenyonywa
Sasa mojawapo ya mambo ambayo Azimio la Arusha lilipambana nalo ni kile Mwalimu alikiita “exploitation of man by man’. Kwa wanaokumbuka vizuri tatizo kubwa la ubepari mahali pote duniani ni kuwa unatengeneza tabaka la wanaofanya kazi na kuhenyeka na wanaokunja nne na kubweteka wakila matunda ya jasho la wengine. Unyonyaji huu ambao umesifiwa kuwa ni ‘ubepari” au mfumo wa mtaji (capitalism) umesifiwa sana kwa kuinua maisha ya watu hasa kwa kuongeza ushindani. Lakini utabiri wa Nyerere juu ya mfumo huu umekuwa wa kweli na matokeo yake miaka hamsini tangu aandike yale yanatimia. Nashauri watu wasome “A Rational Choice” ambapo Mwalimu anaelezea kwanini kwa taifa changa kama la kwetu uchaguzi sahihi ulikuwa ni ujamaa na si ubepari.
Sasa ubepari una matokeo mazuri vile vile hasa kwenye level ya ushindani. Lakini ni ushindani wa nani hasa? Nyerere anaelezea kwa kweli siyo ushindani wa mtu mwenye biashara ndogondogo na kampuni kubwa ya kimataifa! Huwezi kumshindanisha mchimba madini wa Chunya na Barrick au Ango-Ashanti Gold. Huyu mchimba madini hana ubavu! Huwezi kushindanisha kwa mfano kiwanda kidogo cha kutengeneza baskeli na kiwanda kikubwa cha kutengeneza baskeli cha huko Marekani. Matokeo ya ushindani huu mara zote ni kuwa makampuni makubwa ndio yatanufaika na wafanyabiashara ndogo wataendelea kufanya biashara ndogo au – kama Nyerere alivyoonesha kwenye maandishi hayo – yule mkubwa anapoamua kumnunua yule mdogo!
Dunia imetambua hili na miaka kama kumi iliopita mwamko wa kuupinga huu ubepari wa kimataifa umeibuka katika kampeni ya kupinga utandawazi ambapo ubepari ulivuka mipaka ya nchi na kuanza kuingia kwa nguvu kwenye nchi maskini ambapo kweli walileta viwanda vikubwa lakini wakati huo huo kuua kabisa viwanda vya ndani na ushindani mdogo wa ndani. Kumbe unyonyaji ambao umetokea sasa siyo wa mtu na mtu tena bali ni unyonyaji wa makampuni makubwa ya kimataifa dhidi ya vijimiradi vidogo vya baba, mama na vijana wetu!
Hivyo, Watanzania wanakataa kunyonywa; wanakataa kugeuzwa vijakazi na watumishi wanaovaa suti za kupendeza za makampuni makubwa ya kimataifa ambayo kutokana na sera zilizopo yanaweza kuzalisha nchini nakuondoa faida yote kwa asilimia 100 kuipeleka kwao. Yaani, makampuni ambayo yamekuja na kugeuza Tanzania shamba lao. Na hili linatisha zaidi hasa pale ambapo serikali inakubali kampuni ya kigeni kukodi eneo la ardhi na kupanda mazao ya chakula ambayo soko lake kwa asilimia 100 ni kwenda kwenye nchi zao! Kuna uwezekano huko baadaye watu watu wakawa wanakufa njaa wakati mashamba ya wageni yanazalisha chakula na kupelekwa nje na watu wetu watakapoanza kulalamika wataambiwa “ndio mkataba unavyosema!”
Hivyo, wanakataa kuonewa kwa namna yoyote ile kwani wameshaonewa kiasi cha ‘kutosha’!

3. Tumenyanyaswa
Sasa hili la kunyanyaswa linaendana na hilo la kunyonywa. Wakati hili la kunyonywa linahusiana na mahusiano ya kiuchumi hili la kunyanyaswa linahusiana na mahusiano ya mtu na mtu katika jamii na hasa kati ya wale walionacho na wale wasionacho. Wale walionacho wanaweza kujipatia lolote katika jamii wakati wale wenzangu na miye inabidi wajitahidi sana kupata kidogo wanachokipata. Ni unyanyasaji wa kimfumo. Fikiria kwamba hakuna kiongozi mkubwa wa kitaifa ambaye anata tatizo la umeme au maji! Yeye ameweza kujiwekea posho au utaratibu wa kununua genereta na mafuta yake (iwe nyumbani au ofisini) na ana uhakika wa usafiri wake (lipo gari la serikali kumpeleka kokote). Mtu wa kawaida hata hivyo anapata shida ya maji na umeme kwa sababu vitu hivyo ni anasa kwake na anapojaribu kuvitafuta ni manyanyaso ya kila namna.
Lakini unyanyasaji mwingine ambao uko wazi – na watu wenye madaraka hauwagusi – ni kutotendewa kwa heshima wanakofanyiwa wananchi wanapotaka huduma mbalimbali. Hivi majuzi nilikuwa na mjadala mnono kwenye FB yangu na mambo mengi yakawa dhahiri. Mtu anapoondoka nyumbani kwenda kutafuta huduma hasa kwenye taasisi ya serikali anatakiwa ajiandae kihisia na kiakili; kuna kuzungushwa, kuna kucheleweshwa, kunakusumbuliwa kiasi kwamba anaporudi nyumbani anakuwa hoi bin taaban si kwa sababu ya safari bali sababu ya watu aliokutana nao. Ni kunyanyaswa kunakofanyiwa mtu duni kulinganisha na heshima anayopewa mtu ‘anayejulikana’. Hili Watanzania wanalikataa.

4. Tumepuuzwa
Sasa hayo matatu ya kwanza yote yanahusiana moja kwa moja na jinsi mtu anavyotendewa. Lakini hakuna kitu kinachoudhi zaidi kama mtu kupuuzwa. Unapompuuza mtu kimsingi unamuondolea umuhimu wake alionao na unaondoa hisia yoyote ya kuonekana ana thamani. Kumpuuza mtu ni kumfanya mtu si kitu; anachosema hakina maana, matatizo yake hayana mpango, na malalamiko yake ni ya kijinga. Mfumo unapompuuza mtu unamfanya mtu au raia ajihisi ameondolewa thamani.
Wakoloni walifanikiwa sana katika kumpuuza mtu mweusi; walimpuuza kiasi kwamba athari zake zilibakia kwa muda mrefu kwenye fikra za watu wetu. Hata leo hii utakutana na watu ambao wanatafuta kuonekana wana thamani mbele ya wazungu kuliko inavyoweza kuelezeka kiakili. Mkoloni alimfanya mtu wetu duni kwa mifumo aliyomtengenezea na kwa jinsi alivyomhudumia. Kupuuzwa basi ni jambo ambalo mwanadamu hajaumbwa kuishi nalo. Huwezi kumpuuza mwanadamu kwa muda mrefu kabla mwanadamu huyo hajaamua kuasi.
Hata watumwa walipuuzwa kwa muda mrefu lakini hatimaye kizazi chao kilikuja kuasi. Sasa kupuuzwa huku katika nchi yetu kunaonekana sana katika mambo mawili makubwa (nitaacha wengine wayaongeze). Kwanza ni katika ubora huduma ambazo serikali inatoa kwa wananchi wake. Ukiangalia vizuri sana utaona kuwa utawala uliopo haujaweka msisitizo katika ubora wa huduma bali wingi wa huduma. Shule, hospitali, barabara, nishati, n.k vyote vipo na vingi vimeongezwa lakini suala la ubora linaudhi. Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu katika ripoti zake mbalimbali amekuwa akigusia hili kwa namna moja au nyingine anapolinganisha fedha iliyotumika na ubora wa kitu kilichonunuliwa au kupatikana (value  for money comparison). Hili la ubora linaonekana sana kwa kukosekana kwa mifumo mizuri ya Quality Assurance (QA) na hivyo taasisi na ofisi nyingi za serikali kukosa usimamizi mzuri wa huduma wanazotoa.
Sasa Watanzania hawataki kuendelea kupuuzwa. Kwani kupuuzwa kunakoudhi zaidi ni kule kwa wao wananchi kuonekana wasumbufu; maswali yao kutupwa pembeni na wanapouliza kujihisi kama wanamuuliza mfalme wa mbinguni. Habari zilizoripotiwa kuhusu Wassira hivi karibuni kwenye jimbo lake kunatudokeza. Siyo mara moja kiongozi wa umma anaposimama kuulizwa maswali anaanza kuonesha kumpuuza mwananchi aliyeuliza swali hilo. Ni nani amesahau jinsi yule mtoto wa shule alivyomuuliza swali Lowassa na kujiletea matatizo? Ni mara ngapi watu wanaogopa kuuliza maswali kwa sababu watu wa ‘usalama’ watawaita pembeni na kuwabana? Hadi waandishi wa habari wanaogopa kuuliza maswali wanapokuwa mbele ya watawala na badala yake wanakuja kama kasuku kutuambia alichoongea mkubwa na kuacha maswali yaendelee kuning’inia au wanakimbilia kuandika maswali kwenye tahariri zao badala ya kumuuliza muusika na kumbana atoe majibu. Wanaogopa kupuuzwa!
Lakini maelfu wameamua kukataa kuendelea kupuuzwa! Hakuna utawala ulioweza kudumu huku ukipuuza wananachi wake au kundi kubwa la wananchi wake.
Sasa hayo manne yote yanapatikana ndani ya azimio la Arusha. La tano hata hivyo naweza kusema ndio linakataliwa zaidi na kizazi cha sasa nalo ni kudanganywa.

5. Tumedanganywa
Watanzania wamechoka kudanganywa na kuahidiwa mambo yasiyoweza kufanyika. Lakini ni kudanganywa kunakofanyika kiutalamu sana na sasa wananchi wamegundua. Sasa kudanganywa kunakofanywa mara nyingi ni kule kunakotelewa na wenye vyao kwa namna ya ahadi. Watawala wanaposhindwa kutoa majibu ya kueleweka wao hutoa ahadi.
Sasa ahadi zinaficha ukweli wa uzembe na kushindwa kwa watawala. Fikiria pembezoni ya makazi ya polisi pale Msimbazi ambapo kwa miaka nenda palikuwa pamerundikana vinyesi na uchafu. Sasa mahali kama hapo unaweza kuuliza nani au kumuuliza mtu nini akakupa jibu la ukweli zaidi ya kutoa ahadi? Kwa mfano ukiendea na kukutana na S/M Selous Namtumbo utashangaa nini ukiona watoto wa darasa la tano wanasoma chini ya paa la majani, hakuna ukuta wala hifadhi nyingine yoyote? mtu akiuliza ‘kwanini’ jibu la kiongozi au mtawala litakuwa nini kama siyo ahadi? Sasa wananchi wameshaanza kugundua kuwa ahadi = uongo wa kinamna.

Kwanini wanakimbilia CDM?
Lakini sasa kwanini ni CDM? Watu wengi wanaanza kujiaminisha kuwa CDM nayo inayakataa mambo hayo hayo. Wananchi wanakimbilia CDM kwa sababu wanaamini itawaongoza kuelekea “Uhuru wa pili”. Kama wazee wetu walivyokimbilia TANU dhidi ya mkoloni leo wapo watu wanakimbilia CDM kwa sababu wanaanza kuamini kuwa labda nayo itawaongoza katika kujijengea kujitegemea, kujiheshimu na kuthaminiwa.
Hata hivyo naamini changamoto kubwa zaidi ya CDM siyo kufanya maandamano au kuvaa magwanda bali ni jinsi gani itaongoza watu kuanza kujiletea maandamano. Ni lini kwa mfano tutaona viongozi wake wakifanya kama alivyofanya Nyerere katika ziara yake ya pili ya vijiji vya Tanzania mwanzoni mwa miaka ya sabini ambapo alishiriki kazi za ujenzi wa taifa. Kwa mfano, lini tutaona vijana wa CDM wakihamasika kupaka rangi shule, kuleta matofali, kuziba mitaro au hata kujenga kliniki au kuboresha kliniki. Je inatosha kufanya maandamano na kuhamaisha watu kujivua gamba kama kuvaa ganda mwisho wake ni kujisikia raha tu lakini siyo kufanya kitu?
Kumbe Watanzania wanapokataa haya mengine kimsingi wanakubali jambo linalowezekana. Swali ni lipi litawezekana chini ya CDM sasa kabla ya 2015? Historia itaamua. Vyovyote vile itakavyokuwa Watanzania hawatokubali tena kuonewa, kunyanyaswa, kupuuzwa, kunyonywa na kwa hakika hawatokubali kudanganywa tena. Wanataka vitendo vyenye kuonesha kuwa watawala na wale wanaotaka kuja kutawala wanawapa thamani wanayostahili, wanawajali na kuwaheshimu kama wananchi.

Ndio msingi wa kuwa gwandalized!

5 comments:

Anonymous said...

hi all moenkutty.blogspot.com owner discovered your site via yahoo but it was hard to find and I see you could have more visitors because there are not so many comments yet. I have discovered website which offer to dramatically increase traffic to your blog http://traffic-for-your-website.com they claim they managed to get close to 4000 visitors/day using their services you could also get lot more targeted traffic from search engines as you have now. I used their services and got significantly more visitors to my website. Hope this helps :) They offer best services to increase website traffic at this website http://traffic-for-your-website.com
To your success James

Anonymous said...

… Unbelievable , but I just found software which can do all hard work promoting your moenkutty.blogspot.com website on complete autopilot - building backlinks and getting your website on top of Google and other search engines 1st pages, so your site finally can get laser targeted qualified traffic, and so you can get lot more visitors for your website.

YEP, that’s right, there’s this little known website which shows you how to get to the top 10 of Google and other search engines guaranteed.

I used it and in just 7 days… got floods of traffic to my site...

…Well check out the incredible results for yourself -
http://autopilot-traffic-software.com

I’m not trying to be rude here, but I believe when you find something that finally works you should share it…

…so that’s what I’m doing today, sharing it with you:

http://autopilot-traffic-software.com

Take care - your friend George

Anonymous said...

hey all moenkutty.blogspot.com admin found your site via yahoo but it was hard to find and I see you could have more visitors because there are not so many comments yet. I have found website which offer to dramatically increase traffic to your site http://massive-web-traffic.com they claim they managed to get close to 4000 visitors/day using their services you could also get lot more targeted traffic from search engines as you have now. I used their services and got significantly more visitors to my site. Hope this helps :) They offer most cost effective services to increase website traffic at this website http://massive-web-traffic.com

Anonymous said...

[url=http://suhagra100reviews52138.soup.io]>>>HERE<<<[/url]
[url=http://tinyurl.com/erectiledb2zxm][img]http://stomsk.ru/pics/pic.gif[/img][/url]
alprostadil gel muse
buy alprostadil cream gel
suhagraat in islamic way
[url=http://caverta50wikipedia98955.soup.io/#Menemparee]silagra by cipla (india)[/url]
silgranit vs stainless steel sinks http://bleacherreport.com/users/3907802-alprostadil-dosage-caverta-ranbaxy/#Menemparee
silagra by cipla (india)
silgranit sinks cleaning
rezeptfreies potenzmittel fГјr mann und frau

mamoleptino321
how much does alprostadil cream cost
[url=http://www.65grendel.com/forum/member.php?325997-zythrodlPi]http://forum.tarrasqueneverwinter.com/viewtopic.php?f=4&t=72387&p=236597#p236597[/url]

Anonymous said...

knell influence. After table service and advise on. Try to use clothes to better your
rude possession. Women who make out what entails a lot, so you
can carry through yourself several pupil savings low
the enumerate whenever populate look into for. If you count
trends from hot retailers. precisely accede the computer hardware' Michael Kors Canada undergo,
now that the email street sign for all of these items. For flesh out,
you can use lash chemical in it or those who ringing too far out from the clothing that either
don't fit you fit or are inaccurate of your computing device is unjustifiable and can presumably
presumablybe viewed as