BREAKING NEWS;
MADAKTARI 72 WATIMULIWA KAZI MBEYA
|  | 
| Mwenyekiti wa Bodi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Norman Sigara Aikzungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu kufukuzwa kazi kwa madaktari hao | 
|  | 
| 
Mkurugenzi wa wa hospitali ya rufaa Mbeya Dr  E. Sankey akimsikiliza kwa makini kaimu mkuu wa mkoa Mbeya | 
BODI
 ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya, imewasimamisha kazi madaktari 
72 kwa kosa la kutoingia kazini kwa siku tano jambo ambalo ni kinyume 
cha makubaliano ya mkataba.
Imeelezwa
 kuwa madaktari hao ambao 54 ni wale wa mafunzo ambao waliingia mkataba 
wa miaka miwili na hospitali ya Rufaa na madaktari 18 ni wale walioajiriwa na Wizara ya afya.
Akizungumza
 na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Bodi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya 
Norman Sigara, alisema kitendo cha madaktari kutoripoti kazini kwa siku 
tano ni ukiukwaji wa kanuni za utumisha wa umma toleo la 2009 kifungu 
namba F.16-F17 na F. 27.
"Hivyo
 kupitia kanuni hiyo madaktari hao wamesimamishwa kazi na kurudishwa kwa
 mwajiri wao ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa
 hatua zaidi za kinidhamu,"alisema Sigara.
Kwa
 mujibu wa Mwenyekiti huyo wa Bodi, imeelezwa kuwa siku ya tarehe 
23/6/2012 wafanyakazi 15 waliokuwa zamu(Intern Doctors 12 na 
Registrars3) hawakufika kazini na tarehe 24/6/2012 wafanyakazi 19(Intern
 doctors 15 na Registrars 4) hawakufika kazini.
Alisema,
 kuanzia tarehe 25/6/2012 hadi leo imethibitika kuwa Interns doctor 54 
na Registrars 18 hawakufika kazini hadi leo tarehe 28/6/2012 ambapo 
tarehe 25/6/2012 bodi ya hospitali ilifanya kikao cha dharura kujadili 
hali ya utendaji kazi na utoaji huduma hospitalini na kutoa uamuzi.
Sigara,
 aliyataja maamuzi hayo kuwa ni Mwenyekiti wa Bodi akutane na madaktari 
ambao hawakufika kazini ili awasikilize sababu za kutofika na kujadili 
namna ya kumaliza matatizo hayo jambo ambalo madaktari hao waligoma.
Alisema,
 baada ya madaktari hao kukaidi ombi hilo, Bodi ya hospitali ili 
waandikia barua za kujieleza kwanini wasichukuliwe hatua za kinidhamu 
kwa kuvunja mkataba walioingia na hospitali na pia kukiuka kanuni za 
kudumu za utumishi wa umma nalo walilikaidi
"Iwapo
 madaktari ambao hawakuripoti au kueleza sababu za kuridhisha ifikapo 
tarehe 28/6/2012. Kwa kuzingatia kanuni za utumishi wa Umma, madaktari 
hao watasimamishwa kazi na kurudishwa kwa mwajiri wao ambaye ni Katibu 
Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,"alisema.
Aidha,
 alisema kuwa kwa ujumala madaktari hao waligomea barua zote mbili yaani
 ya kuitwa kwenye kikao pamoja na ile ya kuwataka kujieleza hivyo Bodi 
imechukua hatua za kisheria za kuwafukuza kazi.
Hata
 hivyo Mwenyekiti huyo wa bodi, alisema kuwa tayari hospitali ya Rufaa 
kwa ushirikiano wa Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, madaktari watano 
wamepatikana ili kusaidia huduma kwa hospitali hiyo.


 
 
No comments:
Post a Comment