Vituo Ligi Ya Taifa Vyapangwa
Release No. 070
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mei 9, 2012
VITUO LIGI YA TAIFA VYAPANGWA
Kamati
  ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imepanga 
 vituo vitatu vya Ligi ya Taifa inayoshirikisha mabingwa wa mikoa kwa  
ajili ya ligi hiyo itakayoanza Mei 26 mwaka huu.
Kundi
  A lenye mabingwa wa mikoa ya Iringa (Kurugenzi Mufindi), Lindi (Lindi 
 SC), Mbeya (Tenende FC), Morogoro (Mkamba Rangers), Mtwara (Ndanda SC),
  Pwani (Super Star), Rukwa (Mpanda Stars) na Ruvuma (Mighty Elephant)  
zitacheza mechi zake mjini Mtwara.
Mji
  wa Kigoma utakuwa mwenyeji wa mabingwa wa mikoa ya Dodoma (CDA), 
Kagera  (Bandari FC), Kigoma (JKT Kanembwa), Mwanza (Pamba SC), 
Shinyanga  (Mwadui SC), Singida (Aston Villa) na Tabora (Majimaji). 
Kundi
  C lenye mabingwa wa mikoa ya Arusha (Flamingo SC), Dar es Salaam  
(Ashanti United ya Ilala, Red Coast ya Kinondoni na Tessema FC ya  
Temeke), Kilimanjaro (Forest FC), Manyara (Nangwa VTC), Mara (Polisi  
Mara) na Tanga (Korogwe United) watachezea mechi zao mkoani Mara.
Mwisho
  wa kuwasilisha fomu za usajili ni Mei 15 mwaka huu wakati kipindi cha 
 pingamizi ni kuanzia Mei 16 hadi 22 mwaka huu. Mei 23 mwaka huu Kamati 
 ya Mashindano ya TFF itakutana kupitia usajili huo. Wachezaji  
wanaosajiliwa ni wale wale waliochezea timu hizo katika ligi ya mkoa.
Mei
  14 mwaka huu ni mwisho kwa mikoa yenye pingamizi kwa mabingwa wao kuwa
  wameshashughulikia rufani husika. Kamati ya Mashindano imeagiza kuwa 
kwa  mikoa itakayoshindwa kufanya hivyo mpaka baada ya tarehe hiyo 
mabingwa  wao hawatashiriki ligi hiyo.
Timu
  tano zitapanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao. 
Mshindi  wa kwanza kutoka kila kundi na washindwa wawili bora (best 
losers)  kutoka kundi A na C ambayo yana timu nane kila moja.

 
 
No comments:
Post a Comment