KALI YA LEO: BOBAN ASAFIRI KWENDA SUDAN AKIVAA KANDAMBILI
Haruna Moshi Boban akiwa ndani ya kandambili uwanja wa taifa jana. |
Kiungo
mshambuliaji wa timu ya Simba, Haruna Moshi ‘Boban’ jana alikuwa
kivutio kwa mashabiki, wasindikizaji na hata baadhi ya wasafiri
waliomuona wakati wakiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, kuelekea Sudan.
Simba inakwenda Sudan katika mchezo wa marudiano dhidi ya Al Ahli
Shandy utakaopigwa Jumapili ya tarehe 13, mei, 2012 huku ikiwa na mtaji wa ushindi wa mabao
3-0, iliyoupata kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Uvaaji wa
Boban, ndio uliowavutia watu kumtizama, kutokana na kuvaa kama mtu
asiyesafiri.
Boban alikuwa amevaa fulana, suruali ya kimichezo ‘trakisuti’ na
kandambili, hivyo kusababisha watu kuvutika kumuangalia, huku baadhi yao
wakibaki kujiuliza kuhusu vituko vya nyota huyo ambaye mashabiki
humuita Balotteli wa Bongo.
Mchezaji
huyo anafananishwa na mshambuliaji mahiri wa Italia, anayekipiga klabu
ya Manchester City ya England, ambako mara kwa mara amekuwa akibeba
vichwa vya habari katika magazeti ya England na Ulaya kutokana na
vituko vyake.
Ukiondoa
vituko hivyo vya uvaaji wa Boban, msafara wa watu 25 wakiwamo viongozi
watano na wachezaji 20 wa timu hiyo waliondoka chini ya uongozi wa
mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
Hussein Mwamba, majira ya saa 8:00 mchana
(Shaffihdauda.blogspot)
No comments:
Post a Comment