
Mh.
 Balozi. Prof. Anna Tibaijuka akimkabidhi Waziri wa Mawasiliano Sayansi 
na Teknolojia Mh. Prof. Makame Mbarawa anuani iliyo katika  mfumo mpya 
wa anuani ya makazi kwa ajili ya wizara yake.Mfumo mpya wa Anuani za 
Makazi unaonyesha kanda, mkoa, wilaya, kata, mtaa na namba ya nyumba 
hivyo kurahisisha ufikishaji wa huduma za posta kwa wananchi.

 Balozi
 wa heshima wa Anuani za Makazi duniani Prof Anna Tibaijuka (MB) (Wa 
pili kushoto) akisoma anuani ya makazi ya jengo la Mawasiliano muda 
mfupi baada ya kuizindua. Kulia ni  Prof. Makame Mbarawa Waziri wa 
Mawasiliano ,Sayansi na Teknolojia (MB) na Waziri wa Mambo ya Nje na 
ushirikiano wa Kimataifa Mh. Benard Membe (MB) wakishuhudia uzinduzi 
huo.  (Kulia) ni Prof John Nkoma Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya 
Mawasiliano akitoa maelezo kuhusiana na mradi wa Anuani za makazi nchini
 Tanzania .

 Mh.
 Prof. Anna Kajimulo Tibaijuka Balozi wa Heshima wa Anuani za Makazi 
duniani muda mfupi baada ya kutambulishwa rasmi kwa vyombo vya habari 
nchini. Katika hafla hiyo Mh. Balozi, Prof . Anna Tibaijuka aliahidi 
kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha kuwa wakazi wote duniani wanapata 
anuani za makazi.

 Waziri
 wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Benard Camilius Membe 
(MB) akitoa nasaha kwa balozi mteule wa kimataifa wa anuani za makazi 
(hayupo pichani) mara baada ya kutambulishwa rasmi kwa wananchi. Mh. 
Membe kwa niaba ya watanzania alimtakia heri Mh. Balozi. Prof. Anna 
Tibaijuka katika kazi yake hiyo na kumuhakikishia ushirikiano kutoka kwa
 watanzania.

 Mh.
 Balozi. Prof. Anna Tibaijuka (MB) akifanyiwa mahojiano na wanahabari 
walihudhuria kutambulishwa kwake (kushoto) ni Waziri wa Mawasiliano, 
Sayansi na Teknolojia Mh. Makame Mbarawa akishuhudia. Mradi wa mfumo 
mpya wa anuani za makazi unasimamiwa na Wizara ya Mawasilisano, Sayansi 
na Teknolojia chini ya Sekretarieti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania 
(TCRA).

Picha ya pamoja na Mh. Balozi wa kimataifa wa anuani za Makazi.
 
 
No comments:
Post a Comment